Mpendwa kusudi  kesho yako ikuwe ya heri inakuomba ukuwe kwanja umempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

Wakati Kristo anaongoza maisha yako, unakuwa na uhakika kwamba maisha yako itakuwa ya heri. Shetani njo adui wa kwanja wa mwanadamu, kwani ameharibu maisha ya watu wengi ukimupatia nafasi ndani ya maisha yako juu kwamba umeiharibu.

Leo tunawatu ambao wamepanga kuwa watu fulani kesho, sawa wanganga, waalimu wa shule, wa bunge na hata wawaziri alakini leo hawafikii lengo lile kwa sababu walipatia shetani nafasi maishani mwao. Kazi ya shetani ni kuiba, kuchinja na kuharibu na leo ameharibu maisha ya watu wengi.

                   Kitu cha pili chagua vizuri mme ao mke wa maisha yako juu ukachagua vibaya jua kwamba maisha yako yote imeharibika. Leo tuna vijana wengi ambao wameharibu kesho sababu ya kuchagua vibaya, wanachakua sura, uumbile,… na wanasahau kitu kya maana. Tukumbuke mfano wa Amnoni na Tamari, Amnoni alimutamani dada yake na mwisho wakafanya zambi na uangalie kama kesho yao ilikua namna gani. Yale maisha yaliwaletea shida, kijana akamkatala dada na ndungu wa karibu wa dada wakamuua Amnoni.

                   Wakati Mungu aliumba ulimwengu alimuweka mtu katika bustani nzuri ili alichunge na kulitunja.(Mwanzo 1). Ndani ya bustani hii mwanadamu alikua akiongea na Mungu na aliishi na salama pamoja na Mungu na viumbe vyote.

Mbele zambi aingize zambi, Mungu alimupa kutawala kila kitu kilichokua katika bustani, aliruhusiwa kukula matunda ya kila muti ila akaagizwa asile matanda ya mti wa kujua mabaya na mema. Kwa wakati fuu mtu aliishi kwa ushirika pamoja na Mungu na walikua wakiongea kila mangaribi.

                   Mwanadamu alipoasi ushirika wake na Mungu ukakatika kwani alijificha na akasema yeye ni uchi.

                   Sababu tatu ya anguko ya mtu

  1. Tamaa ya Macho

Mti ambao ulikatazwa mwanadamu ulikua wa kupendeza kwa macho, na wakati nyoka alipo mdanganya mwanamuke akatazama mti ule na akautamani kwa sababu ya uziri wake. Na leo tamaa ya macho imeacha vijana wengi wanashindwa kufikia kesho iliyo bora. Sababu ya kutamani vizuri wavionavyo leo wamefikia kuharibu kesho yao. Kuna wengi leo wamakua shuleni alakini sababu ya tamaa wameharibu shule yao kwa kutamani wanawake, pesa hata akili, na hiyo imewasukuma kuingilia mambo ya kishirikina na leo wengi wamekua wendawazimu na wengine wamewaliza shule alakini hakuna kazi.

Wababa wengi wanakua na wake wazuri nyumbani mwao na wanaandaa kesho nzuri alakini sababu ya tamaa ya macho leo wameharibu ndoa zao na kuharibu kesho yao. Kama unapenda uwe na kesho iliyo bora jiepushe na tamaa ya macho.

  • Tamaa ya mwili

Mwanadamu alipotamani mti aliokatazwa ndani ya bustani sasa akatamani aikule. Na walipokula tu zambi ikaingia na ushirika na Mungu ukakatika. Leo watu wangi wanapotamani kwa macho inawasukuma kusanya mambo ambayo inaharibu kesho yao.

  • Kiburi cha uzima

Kiburi cha uzima kiliingia ndani ya mwanadamu na akatamani kuwa kama Mungu. Kwa kweli leo watu wengi wameharibu kesho yao juu ya kiburi cha uzima. Sababu ya sura nzuri, umejiona malkia, hata watu wengine wamekuinua sababu ya uzuri wako na hiyo imekuumbia kiburi cha uzima, umezarau kila mtu hata watumishi wa Mungu umewazarau, kanisani hauendi tena, umesahau gisi uko mavumbi, hapo jua kwamba uko na haribu kesho yako.

Kaka yangu kwa kweli umesoma sana na unakazi nzuri pia umeheshimika sana, ile yote imeumba kiburi ndani yako na umezarau wote ambao unawaona wakienda kanisani na umewaona hawana hakili, kaka yangu ninakuambi kwa kweli wewe mwenyewe uko na haribu kesho yako.

                   Kwa sababu ya kiburi cha uzima watu wengi wameharibu kesho yao, kazi zimeisha, ndoa zimeharibika, maono yamekatika, wengi wamekufa vifo vya haraka sababu tu ya kibu cha uzima.

Wakati anguko ilikua katika bustani mwanadamu alipoteza:

  • Kila kitu kwa sababu ule utawala ambao Mungu alimpatia aliunyanganywa
  • Ushirika wake pamoja na Mungu, yeye ambaye alikua akiongea na Mungu kila jioni alikimbia akajificha

Alakini kwa hayo yote Mungu alionesha upendo wake akamutengenezea nguo kwa ngozi ya kondoo kwa kuwavika. Na tena akamtuma mwana wake wa pekee ili aje akufe kwa msalaba kusudi mwanadamu aokolewe na arudishe ushirika pamoja na yeye. Ninajua mpendwa umeangalia maisha yako na umekata tamaa na umeona kesho yako haina tena tumaini, ninalo lakukuambia ni kwamba usikate tamaa kungali tena tumaini.

Wewe mwenyewe umeangalia mahali unatoka na maisha, unaangalia miradi ambayo ulikua umepanga maishani mwako lakini leo imeshindikana sababu ya zambi, unaangalia unyumba nzuri ambao ulikua nao lakini umeharibika sababu ya zambi na umekata tamaa na hauone tena umuhimu wa kuendelea kuishi, ninakuambia kungali tumaini mpendwa.

Mpendwa usikue miongoni mwa watakao vunjika moyo na kuachana na malengo yako bali tusimame kwani kungali matumaini(Waebrania 10:37-38). Ila ujue kwamba mahali mtu anashindiwaka ni hapo hapo mtu anawezeaka. Mfano wa Josue.

Siri ya kushinda kukata tamaa

  1. Uwe na lengo I Sam 17: 25

Lengo ni kile ambacho mtu huvizia kupata. Saa zingine umeona gisi kesho yako imeharibika sababu ya yale ambayo uliifanya ndani ya ujinga na sasa kusudi kesho yako ikuwe vizuri sharti uwe na malengo. Na ufanye juu chini kukamilisha ile malengo yako na kesho yako itakua ya heri. Daudi aliposikia kwamba goliata ametukana Mungu wa Israeli na amewaogopesha watu wote wa Israeli na kuwa alikua na lengo ya kutengeneza kesho yake akawa na lengo ya kupigana na huyo mu philistini na alipo timiza lengo lake hili akawa amajitengenezea kesho yake. Daudi alisahaulika hata katika jamaa yake wakati Samweli alitumwa na Mungu kupaka mafuta mtoto mmoja wa Yese kusudi awe mfalme, hata alizarauliwa na ndugu zake wakati alitumwa na baba yake ili awapelekee wakubwa wake chakula wakati walikua kwenye vita wakimsikiliza goliata.

  • Uwe na bidii Luka 11:8

Ile ambayo ni lengo itakayo kusaidia tutengeneza kesho yako itumike na bidii. Ukiona Daudi alitumika kwa bidii na mwisho akamuua goliata ambaye watu wote walimuogopa.

Hapa tunakuta mfano wa yule ambaye alikuwa na rafiki ambaye anauzisha mikate na yule ndugu alifikisha wageni usiku na akaona kwamba inamubidi kuenda kwa rafiki yake amupe mikate kusudu wageni wake wapate chakula. Lakini yule wa mikate akakataa kumupatia mikate na akamwambia kwamba ni usiku achunge asubui. Yule akakazana mpaka yule akampatia mikati sababu ya bidii yake. Na wewe mpendwa unakua na malengo kusudi uyafikie ni sharti utumike na bidii sana.

  • Ujitie nguvu kabla haujatiwa moyo na watu I Sam 17: 44-47

Mpendwa usisubiri uanje tiwa moyo na watu njo utatimiza malengo yako kwani unaweza tiwa moyo na watu kumbe na ni kuharibu tena sana malengo yako. Tukiona wakati Daudi aliposikia sauti ya goliata hakukimbia  sawa wengine alakini yeye alikua na lengo ya kumuua na alijitia nguvu na akauliwa ka atafanyiwa nini yule atakaye ua yule mufilistini. Hata kama mufalme alitaka mpa vitu vyake vya vita lakini daudi yeye hakuvikubali sababu alikua na amejitia nguvu na aliviacha.

Mufilistini aliambia Daudi maneno yakumukatisha tamaa na kumuogopesha alakini daudi yeye alikua na lengo na akatumika na bidii kubwa na akajitia nguvu na mwishoni akatimiza lengo lake.

                   Na wewe pia ndugu yangu unapokua na malengo jitie nguvu kwanza na utaweza kufika mwisho hata kama vitisho ni vyingi ukuwe na imani na umutumainie Mungu na utafika ku mwisho.

                   Kusudi kesho ukuwe wa maanauweze kumushinda shetani. Sasa acha tukupatie njia za kumushinda shetani.

  1. Kukimbia Zambi Mwanzo 39:12

                   Kama vile tumenena dhambi ni uasi ao uchafu unao mtenga mtu na Mungu. Kila kitu ambacho kinatia kiambaza kati ya mtu na Mungu.

Tukiona mfano wa Danieli pamoja na ndugu zake hata kama walikua katika mji wa uhamishoni walizingatia malengo yao na kwa mwisho wakaheshimika na hata Danieli akawa mmoja wa mawaziri wa mji huo. Dan 1:11.  Walikua uhamishoni na tena watumwa alakini walikimbia zambi na vitisho vikawa vingi lakini walilinda imani yao na kwa mwisho wakaheshimika ka kesho yao ikawa vizuri.

                   Kuna mifano mingi ndani ya Biblia ya wale ambao walikimbia zambi na kwa mwisho wakakua watu wa maana kesho. Angalia maisha yako mpendwa, unaishi namna gani je umekimbia zambi? Je hauna tamaa ya macho? Hauna tamaa ya mwili? Je hauna kiburi cha uzima? Ni wewe mwenyewe unakua na majibu kwa maswali hayo.

  • Kujitenga na marafiki wabaya

Tukisoma 2 Sam 13: tutakuta pale kijana ambaye alifanya zambi na akaharibu kesho yake na hata akafikia kifo. Alimtamani dada yake Tamari, kwa mwisho ndugu yake Abusaloma akamuua. Kama Amnoni alishindwa ni kwa sababu alikua na rafiki mubaya. Leo tunakuwa na watu wengi ambao wameharibu kesho yao sababu ya marafiki na saa zingine nawe uko miongoni mwao, ile ambayo tunaeza kuambia epuka marafiki mabaya kwani watakuharibishia maisha na ujue kwamba shetani hutumia sana marafiki. Leo tuna wadada ambao wameharibu ubikira wao sababu ya marafiki, wengine ni wajawazito sababu tu ta marafiki wabaya. Kwa hivi anja chunguza kama ni nani aliye rafiki wako.

  •  Kuomba na kusoma Neno la Mungu

Inatubidi tuwe watu wa maombi natuelewe vizuri neno la Mungu, kwani hata Yesu alimushinda shetani kwakumwambia imeandikwa. Kwa kuweza kupigana na shetani inakubidi :

  1. Kulinda maisha matakatifu na kuogopa Mungu
  2. Kuwasamehe wengine
  3. Kufunga chakula
  4. Kuwa na Imani

                   MUNGU AKUBARIKI MPENDWA